“Bongo Movie Kwenda Kwenye Birthday Ya Tiffah Ilikuwa ni Kiki Tu”- Shamsa Ford - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

“Bongo Movie Kwenda Kwenye Birthday Ya Tiffah Ilikuwa ni Kiki Tu”- Shamsa Ford

Msanii wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kupasua kuwa habari ya wasanii wa Bongo movie  kama Wema, Aunty, Shamsa, Faiza, Maimatha na Wolper Kwenda Kwenye party ya Tiffah ilikuwa ni kiki tu.


SIku chache zilizopita Kwenye 40 ya mtoto wa Zamaradi, Babu Tale aliwaalika Bongo Movie kwa ajili ya kwenda South Africa Kwenye party ya Tiffah South Africa Lakini mara moja Zari aliwapiga stop.


Baada ya mgogoro wasanii hao kila mmoja ameonekana kughaili Kwenda huku wengine wakidai kulikuwa hakuna Safari bali ilikuwa ni kiki tu.


Gazeti la Amani, liliamua kuwasaka baadhi ya mastaa waliokuwemo kwenye kamati hiyo ambapo kila mmoja aliongea la kwake kama ifuatavyo;


Faiza Ally alisema kuwa alijua wazi kuwa hatakwenda kwa sababu Zari ‘alishamblock’ siku nyingi kwenye ukurasa wake wa Instagram.Mimi baada ya kutangaziwa vile tu nilijua siwezi kwenda kwa sababu Zari alishaniblock siku nyingi, sasa huwezi kwenda kwa mtu ambaye alishakublock na alivyosema maneno yale ndio kabisaaa”.Maimatha wa jesse alidai kuwa hawezi kwenda kwa sababu hakuipenda tabia ya Zari kuwaambia kuwa watakwenda kumchafulia nyumba.Sikuipenda kabisa tabia ya Zari, yeye angeacha akaona kama kweli tutaenda au la lakini kabla hata siku hajizafika akajibu palepale, ya nini kwenda? Nimemshangaa maana hajui kama kwake tungeenda ingekuwa na faida sana hata kujitangaza kibiashara“.Shamsa Ford yeye alidai kuwa anachojua lile tangazo la wao kwenda Sauz kwenye sherehe ya Tiffah ilikuwa ni kiki tu wala hakukuwa na ukweli wowote.Unadhani mchezo kuwasafirisha watu wote wale, ile ilikuwa ni sehemu ya kiki tu, wala siendi mimi”.


 


The post “Bongo Movie Kwenda Kwenye Birthday Ya Tiffah Ilikuwa ni Kiki Tu”- Shamsa Ford appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source: Ghafla TZRead More