“Bora Kufanya Kazi na Diamond Kuliko Alikiba”-Gigy Money - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

“Bora Kufanya Kazi na Diamond Kuliko Alikiba”-Gigy Money

Video vixen maarufu na Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford kwa jina la usanii Gigy Money amefunguka na kuweka wazi kuwa ni bora kufanya kazi na Diamond kuliko Ali Kiba.


Gigy Money ambaye Hivi sasa anaonekana akiwa amejiunga pamoja na Kundi zima la Wasafi linaloongozwa na Diamond Platnumz ili kushiriki katika tamasha lao la Wasafi Festival.


Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Gigy Money ameibuka na kudai kuwa ameona kuna ubora mkubwa wa kufanya kazi na Diamond kuliko kufanya kazi na hasimu Wake Ali Kiba.Ali Kiba anakunja sana kuliko Diamond  na siku ambayo tulienda kufanya wote shoo Kahama Ali Kiba alinitenga kabisa Backstage”.Wiki mbili zilizopita Diamond Platnumz na Ali Kiba walifanya shoo zao usiku mmoja ambapo Ali Kiba alipiga shoo mkoani Shinyanga/Kahama na Diamond alipiga shoo yake mkoani Mtwara.


The post “Bora Kufanya Kazi na Diamond Kuliko Alikiba”-Gigy Money appeared first on Ghafla! Tanzania.

... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More