BOSI WA ZAMANI WA UDART, ROBERT KISENA AFIKISHWA MAHAKAMANI, ASOMEWA MASHTAKA 19 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BOSI WA ZAMANI WA UDART, ROBERT KISENA AFIKISHWA MAHAKAMANI, ASOMEWA MASHTAKA 19

Na Karama Kenyunko globu ya Jamii. 
Mkurugenzi wa UDART, Robert Kisena (46) na wenzake watatu akiwemo raia wa China,  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka 19 yakiwemo ya utakatishaji na  kusababishia UDART hasara ya zaidi ya BIL. 2.41.
Mbali ya Kisena, washitakiwa wengine ambao wote wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ni Kulwa Kisena (33), Charles Newe (47) na Cheni Shi (32). Raia wa China. 
Katika mashtaka hayo, lipo shtaka moja La kuongoza uhalifu, shtaka moja la kujenga kituo cha mafuta bila kibali,  shtaka moja la kuuza mafuta sehemu zisizoruhusiwa na shtaka la wizi wakiwa Wakurugenzi, 
Pia wanakabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha, mashtaka manne ya kughushi, mashtaka manne ya kutoa nyaraka za uongo, mashtaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na shtaka moja la kuisababishia mamlaka hasara. Washitakiwa hao wamesomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali, George Barasa, Moza Kasubi na Imani Mitume... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More