BREAKING: Bob Wangwe ashinda kesi yake, Wakurugenzi kutosimamia uchaguzi - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BREAKING: Bob Wangwe ashinda kesi yake, Wakurugenzi kutosimamia uchaguzi

Leo tarehe 10 Mei 2019, mbele ya jopo la majaji watatu lililoongozwa na Jaji Atuganile Ngwala, limetoa hukumu iliyompa ushindi mlalamikaji Bob Chacha Wangwe, kwenye kesi yake dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Attorney General), Mkurugenzi wa chaguzi za taifa na Tume ya Uchaguzi wa Taifa; juu ya vifungu vya sheria ya uchaguzi wa taifa vinavyotoa mamlaka kwa Wakurugenzi ambao ni watumishi wa Umma, kusimamia chaguzi.Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Uchaguzi wa Taifa inatakiwa kuwa huru na wasimamizi wake hawatakiwi kujihusisha na vyama vya siasa. Hivyo maamuzi ya kesi hiyo yametupilia mbali ushahidi uliotolewa na upande wa washtakiwa.


Aidha, Jaji Ngwala ameushauri upande wa washtakiwa kukata rufaa ya uamuzi huo katika mahakama ya rufaa endapo hawajaridhika nao.


Chanzo: Loveness Muhagazi, Watetezi TV,


The post BREAKING: Bob Wangwe ashinda kesi yake, Wakurugenzi kutosimamia uchaguzi appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More