BREAKING NEWS:: WAZIRI DK. MWIGULU NCHEMBA AMSIMAMISHA KAZI MSAJILI WA TAASISI ZA KIDINI WIZARANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BREAKING NEWS:: WAZIRI DK. MWIGULU NCHEMBA AMSIMAMISHA KAZI MSAJILI WA TAASISI ZA KIDINI WIZARANI

*Wizara yake yaanza kumchunguza aliyesambaza nyaraka na matamko mitandaoni 
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba ametangaza kumsimamisha kazi Msajili wa Taasisi za kidini Maryline Komba, huku akiwaomba viongozi wa dini kuendelea na shughuli zao za kutoa huduma za kiroho.
Pia amesema kwa sasa Wizara yake inaendelea kuchunguza aliyeandika na kusambaza nyaraka katika mitandao ya kijamii ambayo imeibua sintofahamu kwa viongozi wa dini mbalimbali na Watanzania kwa ujumla ili sheria ichukue mkondo wake.
Ameongeza kuwa viongozi wa dini na watanzania kwa ujumla wafahamu kuwa nyaraka na matamko ambayo yamesambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina baraka za Wizara husika wala Serikali na hivyo ni vema zikapuuzwa tu.
"Tuwaombe viongozi wa dini kupuuza nyaraka ambazo zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Endeleeni na shughuli zenu kama kawaida kwani nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba na hivyo msiwe na hofu.
"Serikali na viongozi wa dini wamekuwa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More