BREAKING NEWSSS: KING MAJUTO HATUNAYE TENA, AFARIKI DUNIA USIKU HUU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BREAKING NEWSSS: KING MAJUTO HATUNAYE TENA, AFARIKI DUNIA USIKU HUU

Msanii mkongwe  Amri Athuman maarufu kama " King Majuto"  amefariki dunia usiku huu katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa mara tu baada ya kurejea nchini kutoka nchini India alikopelekwa na serikali kwa matibabu.Msanii maarufu mhekeshaji Joti ndiye alikuwa mtu wa kwanza kutoa taarifa hizo za kusikitisha katika mtandao wake wa Instagram, ikiambatana na picha yake akiwa na msanii Mpoki walipokwenda kumjulia hali hospiali.Joti ameandika kwenye ukrasa wake wa Instagram: “R.I.P @Kingmajuto. metuachia Maumivu Makubwa sana ktk Tasnia ya Comedy Tanzania Sisi wanao,Tutakukumbuka kwa kazi zako,Upendo wako,Tabasamu lako Daima milele,Tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi,Pumzika kwa Amani Mzee wetu,” ameandika Joti.Mwigizaji nyota wa vichekesho Steve Nyerere naye kwa masikitiko makubwa amethibitisha habari hiyo kwa kusema: "Kweli kaka, Mzee wetu katutoka. Tunalia kwa kumpoteza Mzee wetu..."Muigizaji huyo alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na k... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More