BREAKING NEWZZZ:MSANII MAARUFU WA BONGOFLEVA AFARIKI DUNIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BREAKING NEWZZZ:MSANII MAARUFU WA BONGOFLEVA AFARIKI DUNIA

Hivi punde chumba cha habari Globu ya Jamii imepokea taarifa za kusikitisha/huzunisha  zinazohusu aliyekuwa Msanii mahiri katika miondoko ya kughani a.ka Rap almaarufu kwa jina la Godzilla amefariki Dunia.
Taarifa zinaeleza kuwa Msanii huyo maye kwa jina halisi anaitwa Golden Mbunda,aliyekuwa akitikisa anga ya bongofleva katika miondoko ya hip hop nchini ,amefariki Dunia ghafla  usiku wa kuamkia leo Jumatano Februari 13,2019 akiwa nyumbani kwao maeneo ya Salasala,jijini Dar.
Mwili wake umepelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Lugalo,Mwenge.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi-AMIN.
TUTAENDELEA KUWAJUZA HABARI ZAIDI KADIRI ZITAKAVYOKUWA ZIKIINGIA.... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More