BREAKING NEWZZZ: MWIGIZAJI KING MAJUTO AFARIKI DUNIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BREAKING NEWZZZ: MWIGIZAJI KING MAJUTO AFARIKI DUNIA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli siku waliopokwenda kumjulia hali King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam  Januari 31, 2018.

Msanii mkongwe  Mzee Amri Athuman al maarufu kama " King Majuto"  (pichani, enzi za uhai wake) amefariki dunia usiku huu katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa mara tu baada ya kurejea nchini kutoka nchini India alikopelekwa na serikali kwa matibabu.
Afisa habari wa Chama cha Filamu na Waigizaji, Masoud Kaftany, amethibitisha kifo cha King Majuto, wakati msanii maarufu mchekeshaji Lucas Lazaro Mhuvile maarufu kama Joti ameandika msiba huo katika mtandao wake wa Instagram, ikiambatana na picha yake akiwa na msanii Mpoki walipokwenda kumjulia hali hospiali.

Joti ameandika kwenye ukrasa wake wa Instagram: “R.I.P @Kingmajuto. metuachia Maumivu Makubwa sana ktk Tasnia ya Comedy Tanzania Sisi wanao,Tutakukumbuka kwa kazi zako,Upendo wako,Tabasamu lako Daima milel... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More