BREAKING NEWZZZZZ: KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AFANYA MABADILIKO MAKUBWA YA WAKUU WA MIKOA WA JESHI HILO TANZANIA BARA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BREAKING NEWZZZZZ: KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AFANYA MABADILIKO MAKUBWA YA WAKUU WA MIKOA WA JESHI HILO TANZANIA BARA

Katika kuboresha utendaji kazi ndani ya Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Martin Kasike amefanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi kwa kuwateua Wakuu wa Magereza wa Mikoa Tanzania Bara(RPOs) 19 wapya na saba (7) kuwabakiza katika nyadhifa zao. Katika mabadiliko hayo Kamishna Jenerali Kasike ameteuwa na kuthibitisha maafisa sita (6) kuwa Wakuu wa Vyuo vya Magereza na kuwabadilisha maafisa wengine watatu (3) katika vitengo muhimu ndani ya Jeshi hilo. Aidha, Kamishna Jenerali Kasike katika mabadiliko hayo kwa mara ya kwanza amewateua Wakuu wa Magereza wa Mikoa katika mikoa ya Katavi, Songwe, Njombe, Simiyu na Geita ambayo ilikuwa haina uongozi wa kimagereza katika ngazi ya mikoa hiyo. Katika mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa RPO (DSM) SACP. Hamis Nkubasi ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kitengo cha Ujenzi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP. Julius Ntambala, SACP. Salum Hussein RPO (Dodoma) amebakia katika kituo chake na aliyekuwa Mkuu wa Ch... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More