Breaking: Sakata la uchaguzi Yanga, kamati ya utendaji yaitisha ghafla mkutano mkuu wadharura - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Breaking: Sakata la uchaguzi Yanga, kamati ya utendaji yaitisha ghafla mkutano mkuu wadharura

Kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga imeamua kuhitisha mkutano mkuu wa dharura utakao fanyika tarehe 24 ya mwezi huu wa 11.Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram Yanga imetoa taarifa hiyo huku ikiwa zoezi la kuchukua fomu za kuwania nyadhifa mbalimbali ndani ya klabu hiyo zikiendelea.


Wakati uchaguzi mkuu wa Yanga ukitarajiwa kufanyika tarehe 13 ya mwezi Januari hapo mwakani kupitia kwa mwenyekiti wa baraza la wadhamini ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika hapo jana siku ya Jumapili ametanabaisha kuwa aliyekuwa mwenyekiti wao, Yusuf Manji bado anaendelea kushikilia kiti hiko kwa mujibu wa barua waliyoipokea kutoka kwake.


“Kwenye mkutano mkuu ule wa wanachama, ilipigwa kura nani wanamtaka Manji arudi, wajumbe wote 4500 walisema tunamtaka Manji arudi na sisi katika baraza la wadhamini tukasema Manji aandikiwe barua “, amesema Mkuchika.


George Mkuchika ameongeza “Tukamuandikia barua na ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More