Brown Akanusha Kukimbia Mombasa Baada Ya Kuiba Mke Wa Mtu - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Brown Akanusha Kukimbia Mombasa Baada Ya Kuiba Mke Wa Mtu

Msanii wa muziki kutoka Mombasa Kenya, Brown Mauzo ameibuka na kukataa yuhuma zinazomkabili za kukimbia Mombasa na kuja Dar Es Salaam baada Ya kuiba mke wa mtu.


Tuhuma hizo za Brown kukimbia Mombasa zilitolewa na msanii mwenzake anayeitwa Kelechi ambaye alidai Msanii huyo alikimbilia Dar kutoka Mombasa baada ya kutembea na mke wa Meneja wake.


Kwenye mahojiano na Kipindi cha Enews cha East Africa Tv, Brown amekataa tuhuma hizo na kusema yeye na Meneja wake wapo vizuri kabisa na hajaiba mke wake wala hajakimbia Mombasa.Yaani hakuna kitu kama hicho kama sio naweza kupiga simu hata saa hii kwa meneja wangu niongee naye, hayo ni maneno watu tu wanazungumza yaani hilo jambo ndio kwanza nalisikia sasa hivi”.Lakini pia Brown amesisitiza kuwa yeye yupo hapa Dar kwa muda na nyumbani Kenya anaweza kurudi lakini sio kwamba amefukuzwa kwa sababu ya kuiba mke wa Meneja wake.


The post Brown Akanusha Kukimbia Mombasa Baada Ya Kuiba Mke Wa Mtu appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More