BSS YANOGA KUPITIA STARTIMES - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BSS YANOGA KUPITIA STARTIMES

SHINDANO la kusaka vipaji vya muziki maarufu kama  BSS limeendelea kunoga kupitia StarTimes Swahili.
 Akizungumza na vyombo vya habari Meneja masoko wa Startimes Davis Malisa amesema kuwa "kwa mara ya kwanza katika historia ya Bongo Star Search, itakuwa ikiruka kila siku kupitia chaneli yao ya Kiswahili, (ST Swahili) saa 3 Usiku, na hii ni kuwapa fursa ya  kutazama maudhui mengi zaidi ambayo wamekuwa wakiyakosa katika misimu iliyopita” ameeleza Malisa.
Imeelezwa kuwa shindano la Bongo Star Search limeingia katika msimu wake wa tisa baada ya mapumziko na mafanikio makubwa kwa misimu minane tangu kuanzishwa kwake. Pia ni shindano kubwa zaidi la vipaji kuwahi kufanyika nchini Tanzania, kwa mwaka huu shindano hilo linarushwa kupitia king’amuzi cha StarTimes na chaneli yao ya StarTimes Swahili ikiwa ni mara ya kwanza kwao kufanya hivyo.
“Tuna shauku kubwa sana kuwaletea maudhui haya ambayo kwa takribani miaka miwili watazamaji wa luninga wameyakosa, BSS ni shindano la kipekee na ambalo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More