BWENI LA SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI LATEKETEA KWA MOTO LEO ASUBUHI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

BWENI LA SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI LATEKETEA KWA MOTO LEO ASUBUHI

 Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
BWENI la wavulana katika  Shule ya Sekondari Mlangarini ambayo ni shule ya Serikali  iliyo katika kata Mlangarini Halmashauri ya Arusha Wilaya ya Arumeru limeungua moto.
Taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Jerry Muro amesema leo Januari 12,2019 amepata taarifa za kuungua kwa bweni saa moja asubuhi.
Amesema taarifa za awali zinaeleza moto huo ulianza Alfajiri na kuteketeza chumba kimoja kati ya vyumba 14  vya bweni hilo lililokuwa na wanafunzi 84 na kwamba hakuna majeruhi wala vifo.
"Japo kuna uharibifu wa mali ikiwemo kuungua kwa  vitanda (double) vitatu (3),magodoro (6),Masanduku ya kuhifadhia nguo na madaftari.      Kutokana na changamoto hiyo nililazimika kufika eneo la tukio mapema na kuungana na wanafunzi pamoja na wananchi waliojitokeza katika hatua za awali ambapo pia kikosi cha Zimamoto kiliwahi kufika kwenye eneo la tukio na kukuta moto umezimwa kwa ( fire extinguisher 11)," amesema Muro.       
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru m... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More