CAF YAIVUA CAMEROON UENYEJI WA AFCON KWA MAANDALIZI DUNI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CAF YAIVUA CAMEROON UENYEJI WA AFCON KWA MAANDALIZI DUNI

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeipokonya Cameroon uenyeji Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa sababu haijaridhishwa na maandalizi yao.
Taarifa ya CAF jana imesema kwamba maamuzi hayo yamechukuliwa katika kikao cha Kamati Kuu ya shirikisho hilo kilichofanyika mjini Accra, Ghana juzi.
Maamuzi hayo ambayo hayana nafasi ya rufaa, yanamaanisha sasa CAF itafungua milango kwa mwenyeji mwingine wa mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika katikati ya mwakani.

Sasa tiketi ya Cameroon kwenda kutetea Kombe la AFCON ipo kwa Comoro

CAF imeahidi kumtambulisha mwenyeji mpya wa AFCON ifikapo Desemba 31, mwaka huu huku Cameroon ikipewa kipaumbele katika uenyeji wa fainali zijazo.
Isingepokonywa uenyeji, Cameroon ingeandaa michuano ya AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1972.
Simba Wasiofungika wa Cameroon kwa sasa ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kutwaa Kombe hilo kwa mara ya tano kihistoria katika michuano iliyopita wakiifunga Misri 2-1 katika fainali Uwanja wa L'Amitie mji... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More