Caf yakanusha taarifa za kunyimwa visa Rais Ahmad Ahmad kuingia Marekani, ili kushiriki mkutano wa FIFA - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Caf yakanusha taarifa za kunyimwa visa Rais Ahmad Ahmad kuingia Marekani, ili kushiriki mkutano wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika (Caf), kupitia tovuti yake limesema kuwa limeshangazwa na habari iliyoenezwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii kuwa Rais Ahmad Ahmad amenyimwa visa ya kuingia nchini Marekani kushiriki mkutano wa Shirikisho la soka duniani FIFA unaonza kufanyika Machi 15 mwaka 2019 huko Miami.

Caf imesema kuwa imeshangazwa na kuvumishwa kwa habari hizo za uongo pasipo kutaka kuthibitisha ukweli.

Hata hivyo shirikisho hilo lenye dhamana ya kusimamia maendeleo ya soka la bara la Afrika limewathibitishia wanafamilia kandanda katika bara hili kuwa hakuna wakati wowote umewahi kutokea kwa Rais Ahmad Ahmad kunyimwa visa ya kuingia Marekani.

Huku likisema kuwa Rais huyo ni kama wanachama wengine wa FIFA, visa yake hushukhulikiwa na kutolewa na ubalozi wa Marekani nchini Misri.

Na kuongeza kuwa Rais hueshimu sheria na taratibu zote za upatikanaji wa visa, na hukubaliana na kanuni za kila nchi.

Kwa taarifa hiyo ya Caf inaonyesha dhahiri k... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More