CAF YAWAPIGA CHINI MAREFA WA TANZANIA AFCON 2019, YACHUKUA HADI WA BURUNDI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CAF YAWAPIGA CHINI MAREFA WA TANZANIA AFCON 2019, YACHUKUA HADI WA BURUNDI

Na Mwandishi Wetu, CAIRO
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya marefa 27 na marefa wasaidizi 29 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka huu nchini Misri, lakini hakuna Mtanzania hata mmoja.
Waamuzi hao wameteuliwa kushiriki kozi maalum kuanzia Aprili 28 hadi Mei 5 mwaka huu mjini Rabat, Morocco kunolewa kwa ajili ya Fainali za Misri mwezi Juni.
Marefa hao wanatoka nchi 33 na wataingia kwenye kambi maalum ya mafunzo itakayosaidia uteuzi wa orodha ya mwisho ya marefa watakaochezesha fainali za mwaka huu zitakazoanza Juni 21 hadi Julai 19 katika miji ya Alexandria, Cairo, Ismailia na Suez.
Florentina Zabron, mmoja wa marefa waliochezesha mechi nyingi msimu huu Tanzania

Wakiwa mjini Rabat, kwanza marefa hao watafanyiwa vipimo vya afya kabla ya kufanyishwa mtihani wa utimamu wa miili chini uya usimamizi wa wakufunzi wazoefu wa CAF. 
Baada ya hapo wataingia darasani kwa majadiliano ya sheria za mchezo, ambayo yataanza Juni 1 ambazo zitakwenda kutumika kwenye m... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More