CAG Prof. Assad “Nitaitikia wito wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maadili na Madaraka” - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CAG Prof. Assad “Nitaitikia wito wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maadili na Madaraka”

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali Prof Mussa Asad amekiri kuwa ataitikia wito wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maadili na Madaraka ya Bunge January 21 2019, Prof Asad amepokea wito rasmi wa maandishi January 15 2019

Prof Assad ametoa kauli hiyo ikiwa ni wiki chache toka Spika wa Bunge, Job Ndugai kumtaka mkaguzi huyo kwenda kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maadili na Madaraka ya Bunge kwaajili ya kuhojiwa kufutia kauli yake ambayo ilitafsiwa kwamba amesema Bunge ni dhaifu.

“Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Bunge ni Taasisi ambazo lazima zielewane na kufanya kazi kwa karibu sana, kwa imani yangu nina mahusiano mazuri na Bunge”, CAG Prof. Mussa Assad

Aliongeza, “Majibu yangu katika mahojiano yaliyozua mjadala hayakuwa na nia ya kulidhalilisha Bunge hata kidogo, maneno kama udhaifu ni lugha ya kawaida sana kwa Wakaguzi kutoa maoni ya utendaji wa mfumo wa taasisi mbalimbali”


The post CAG Prof. Assad “Nitaitikia wito wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maadili... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More