CANADA KWA USHIRIKIANO NA SERIKALI YA TANZANIA YAENDESHA MAFUNZO YA MRADI WA KUKUZA AJIRA KWENYE SEKTA YA UFUNDI STADI NCHINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CANADA KWA USHIRIKIANO NA SERIKALI YA TANZANIA YAENDESHA MAFUNZO YA MRADI WA KUKUZA AJIRA KWENYE SEKTA YA UFUNDI STADI NCHINI

Na Ahmed Mahmoud ArushaSerikali za Canada na Tanzania zinaendesha mradi wa miaka mitano wenye lengo la kusaidia vijana kuweza kuwa na umahiri wa kujiajiri na kujifunza kwa kutenda.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa vyuo vya ufundi nchini Dkt.Noel Mbonde wakati akifungua semina ya mradi huo inayoendelea jiji Arusha na kubainisha kuwa mradi huo utafikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa Kati wa viwanda.
Amesema kuwa mradi huo ulionza mwaka 2014 unatarajiwa kufika tamati Machi mwakani utasaidia Sana vijana kwani unalenga kumuwezesha kijana na mwalimu kuwa karibu na umeleta mabadiliko chanya nchini.
"Serikali imejipanga kuhakikisha mradi huu unakuwa endelevu baada ya kumalizika kwani tuna miradi mingi inaendeshwa nchini yenye lengo la kuongeza weledi kwa vijana wetu kuweza kufikia adhma ya serikali ya uchumi wa Kati wa viwanda"alisema Dkt.Mbonde.
Kwa upande wake mwakilishi wa Balozi wa Kanada nchini Tanzania bi Nathalie Garon amesema kuwa serikali ya nchi yake itaendeleza ushirikia... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More