CANADA YAHALALISHA MATUMIZI YA BANGI HADHARANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CANADA YAHALALISHA MATUMIZI YA BANGI HADHARANI

HATIMAYE Canada imeandika historia baada ya kuwa nchi ya pili duniani baada ya Uruguay kwa kuhalalisha rasmi matumizi ya bangi hadharani kama dawa na starehe.   Jarida la Times nchini humo limeeleza kuwa baada ya miaka 95 ya kuzuiliwa kwa matumizi ya bangi hatimaye Canada imetangaza rasmi matumizi ya bangi na soko la kuuza bangi lilifunguliwa rasmi usiku wa kuamkia jumatano. Na hiyo imekuja baada ya watu zaidi ya milioni 15 kutoa maoni yao katika sanduku la posta na kupendekeza uhalalishaji wa matumizi ya bangi. 
Imeelezwa kuwa mwaka 2001 bangi iliruhusiwa kutumika kama dawa na hiyo ni baada ya shinikizo kutoka kwa wabunge nchini humo na kwa sasa watatununua na kutumia bangi hadharani bila bughudhi na polisi watahakikisha na kukabiliana na visa vya uendeshaji magari wakiwa wamelewa bangi. Uhalalishwaji huo umekuja baada ya ahadi ya waziri mkuu wa nchi hiyo Justin Trudeau wa Liberal Party of Canada katika kampeni zake za mwaka 2015. 
Na baadhi ya wananchi wameonekana ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More