CASTLE LAGER YAMLETA SAMUEL ETO'O NCHINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CASTLE LAGER YAMLETA SAMUEL ETO'O NCHINI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya JamiiKAMPUNI ya bia ya Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Castle lager imemualika mmoja ya wachezaji bora barani Afrika Samuel Eto'o kuzindua mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira aina ya 5-A-side utakaojengwa Oysterbay jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa bia hiyo Pamela Kikuli amesema kuwa nyota huyo atashiriki katika uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa uwanja maalumu wa soka linaloshirikisha wachezaji kumi (watano kila upande) maarufu kama ‘5-A-Side soccer’ katika eneo la Oysterbay  mkabala na jengo la Coco Plaza, jirani na ufukwe wa Coco.
 
Aidha ameeleza kuwa lengo la kumleta nguli huyo wa soka barani Afrika ni kuongeza hamasa ya soka kwa wanamichezo wenye vipaji kujitokeza kushiriki katika kabumbu.
Pia amesema kuwa kama kampuni wataendelea kushiriki katika shughuli za kijamii katika kuleta maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake msemaji ya klabu ya Simba  amesema kuwa urafiki unasimama hasa katika wakati wa ku... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More