Castle Lager yawafungulia bonge la fursa wachezaji Bongo - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Castle Lager yawafungulia bonge la fursa wachezaji Bongo

Mashindano ya Castle Lager 5 msimu wa pili yamezinduliwa rasmi leo Afrika Kusini katika jiji la Johannesburg ambayo ni mashindano ya mpira wa miguu yanayoshirikisha wachezaji watano watano.


Katika msimu wa kwanza nchi 5 zilishiriki ambazo ni Zambia, Afrika Kusini, Tanzania, Eswatini na Zimbabwe na kushuhudia Afrika Kusini ikitwaa ubingwa huo katika fainali zilizofanyika Zambia.


Mwaka huu Castle Lager 5 imeongeza washiriki kutoka watano hadi nane huku fainali zake zikitarajia kufanyika hapa nchini.


Maneja wa bia hiyo Pamela Kikuli amesema, kufanyika kwa mchezo huo Tanzania ni fursa ya kukuza mchezo huo hapa nchini huku balozi wa mchezo huo Tanzania Ivo Mapunda akielezea tofauti ya mwaka jana na mwaka huu.


“Mwaka jana mashindano hayakuwa na nguvu sana kama mwaka huu, mwaka huu kuna nyongeza ya nchi shiriki ikiwa ni mapona na Ghana na Uganda kwa hiyo tutakuwa na nchi nyingi na ushindani utakuwa mkubwa”-Ivo Mapunda.


“Ni afasi kwa wachezaji wanaochipukia kuja kuonesha vipaji vyao na w... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More