Casto arudi kwa style hii, wasanii na wadau wampokea na kumsifu! - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Casto arudi kwa style hii, wasanii na wadau wampokea na kumsifu!

Baada ya ukimya wa wiki moja, Casto Dickson Jumatato hii amepost picha yake ya kwanza ikawa ni siku 4 toka mtoto wa Muna, Patrick Peter ambaye alikuwa akidaiwa ni wake azikwe katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.


Mtangazaji huyo wa kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV, hakuweza kuzungumza chochote wala kuonekana toka msiba huo utokee licha ya aliyekuwa mpenzi wake, Muna kudai mtoto huyo alikuwa ni wake na sio wa Peter Komu ambaye alikuwa mume wake wa ndoa.


Kauli hiyo ya Muna iliwasha moto upande wa familia ya Peter ambapo ilidai kwamba itakwenda mahakamani kama mrembo huyo asingekubali kutoa mwili wa mtoto huyo ili wamzike kwa kuwa ni mtoto wao na wanavielelezo vyote.


Baada ya kauli hiyo Muna ambaye alikuwa nchini Kenya pamoja na mwili wa marehemu, aliamua kukubali kutoa mwili wa mtoto huyo na kushirikiana na familia ya Mzee Peter kwaajili ya mazishi na kuzikwa Jumapili hii katika makaburi ya Kinondoni.


Kupitia Instagram, Casto amepost picha yake ya kwanza na kuonyesha kums... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More