Casto Athibitisha Ndoa Hivi karibuni. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Casto Athibitisha Ndoa Hivi karibuni.

Mtangazaji kutoka clouds media Casto Dickson ambae alivuma sana baada ya kuingia katika mapenzi na mwanadada Tunda video vixen lakin baadae kuonekana kulega lega kwa penzi hilo hata kusemekana kuwa waili hao kwa sasa wameachana amefunguka na kusema kuwa anakaribia kufunga ndoa.


Maneno hayo yanaleta mshangao mkubwa kwa sababu kila shabiki yake anataka kujua kuwa mwanamke anaefunga nae ndoa atakuwa ni nani  kwa sababu wengi wanajua kuwa ameachana na Tunda.


Hata hivyo alipokuwa akiongea na Millard Ayao , Casto hakutaka kusema ni mwanamke gani anafunga aneo ndoa zaidi ya kusema kuwa anakaribia kufunga ndoa hivi karibuni.


Hata hivyo wawli hao wanaonekana bado kuwa pamoja hasa katika kipindi hiki ch karibuni baada ya Casto kuweka picha katika mtandao huku akimsifia mpiga picha kuwa ni Tunda.


Casto aliwahi kutangaza kuwa anatarajia kufunga ndoa na mwanadada huyo hapo siku za nyuma.


The post Casto Athibitisha Ndoa Hivi karibuni. appeared first on Ghafla! Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More