CBA waadhimisha miaka 10,Dk Mengi awataka kusaidia kipato cha chini - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CBA waadhimisha miaka 10,Dk Mengi awataka kusaidia kipato cha chini

Na Mwandishi wetuMWENYEKITI Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi ameitaka benki ya biashara ya CBA kuendelea kuwawezesha watanzania, hususani wa chini wapatao milioni  7.5 kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.Dk. Mengi alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati wa maadhimisho ya miaka 10 ya benki hiyo mjini Dar es salaam ambapo yeye ndiye alikuwa mgeni rasmi.Pamoja na historia ndefu ya benki hiyo ilivyoanzishwa na baadae kuhamishia makao yake makuu mjini Nairobi, Kenya, Dk. Mengi alisema benki hiyo ina wajibu mkubwa wa kuwezesha kundi kubwa la watanzania kuukataa umaskini.Dk. Mengi ambaye ametoa kitabu kinachoonesha jinsi ya kukabiliana na umaskini na ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF, amesema amevutiwa na mpango wa Benki hiyo wa kuwapatia mikopo watu wa kawaida sana kupitia mpango wake wa kuweka akiba kupitia simu za mikononi ujulikanao kama M- Pawa.Alisema anaamini kama benki imedhamiria na kujiamini wanaweza kujipatia mafanikio makubwa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More