CCM IRINGA WAPATA MWENYEKITI MPYA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CCM IRINGA WAPATA MWENYEKITI MPYA

NA DENIS MLOWE, IRINGA

CHAMA cha Mapinduzi mkoa wa Iringa, kimemchagua mwadhili wa chuo kikuu cha Ruaha mkoani hapa, Dk. Abel Nyamahanga kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho kuchukua nafasi ya mwenyekiti aliyejiuzulu ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila.

Wajumbe 597 kati ya 631 waliohudhuria wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti mpya wa chama hicho chini ya msimamizi wa uchaguzi aliyekuwa waziri mkuu awamu ya nne, Mizengo Pinda.

Mkutano huo maalum uliohudhuriwa na wadau mbalimbali mkoani hapa ulikuwa wa upinzani mkali ambapo kutokana na wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM mkoa kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM wajumbe wote ni 631.

Wajumbe hao walitakiwa kuwapigia kura wanachama watatu ambao ni Vitusi Mushi, Amani Mwamwindi na Dk. Abel Nyamahanga ambao majina yao yalirudishwa kutoka kamati kuu ya CCM taifa kwa leng... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More