CCM WAFUNGA KAMPENI KIBABE JIMBO LA UKONGA,DK. BASHIRU ATOA MSIMAMO KWA WANANCHI,AELEZA NAMNA WALIVYOJIPANGA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CCM WAFUNGA KAMPENI KIBABE JIMBO LA UKONGA,DK. BASHIRU ATOA MSIMAMO KWA WANANCHI,AELEZA NAMNA WALIVYOJIPANGA


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimehitimisha kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam kwa kuwahakikishia wananchi yote yaliyoahidiwa yatatekelezwa na hakuna wa kuwarudisha nyuma.
Wakati wa kuhitimisha kampeni hizo leo mamia ya wananchi wa Jimbo la Ukonga wamejitokeza kwa wingi huku Katibu Mkuu wa CCM  Dk.Bashiru Alli akiweka wazi kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Dk.John Magufuli amefanikiwa kudhibiti ugonjwa uliokuwepo wa baadhi ya wanachama  kutumia rushwa ili kupata uongozi
Akizungumza mbele ya maelfu ya  wananchi wa jimbo hilo Dk.Bashiru amewaomba wamchague mgombea ubunge wa CCM Mwita Waitara kwani ndio mtu sahihi huku akieleza namna ambavyo Chama hicho kimejipanga katika kuwatumikia wananchi hasa katika kuwaletea maendeleo. Ameeleza miradi  namna mikubwa ya maendeleo inavyoendelea kutekelezwa na kwamba anawashangaa wanaodai uchumi umedorora.
Hivyo Dk.Bashiru amewaomba wananchi hao kumchagua Waitara kwa ajili ya kushiriki kikamilif... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More