CCM Watoa TAMKO Kuhusu Malumbano ya Benard Membe na Katibu Mkuu wa Chama Hicho - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CCM Watoa TAMKO Kuhusu Malumbano ya Benard Membe na Katibu Mkuu wa Chama HichoChama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wana CCM na watanzania kuhusu matokeo ya uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata 47 Tanzania Bara uliyofanyika tarehe 02 Desemba 2018 na kwamba CCM imepita bila kupingwa katika Kata 41 na katika Kata 6 ambako kumefanyika uchaguzi CCM imeshinda kwa kishindo.
Katika chaguzi hizi ambazo CCM imeendelea kuongoza inajivunia umakini mzuri wa kufuata Taratibu, Kanuni na Sheria za Nchi yetu, Sera nzuri, ahadi zinazotekeleka na siasa safi na uongozi bora.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuwashukuru watanzania na wanaCCM wote kwa kuendelea kukiamini na kukichagua na kwamba CCM itaendelea kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa haraka katika maeneo yao.
Aidha Chama kinapenda kuwafahamisha kuwa tarehe 17 hadi tarehe 18 Desemba 2018 Jijini Dar es salaam kutakuwa na vikao vya Chama vya kawaida vya Uongozi Taifa ambapo tarehe 17 Desemba 2018 kutakuwa na Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na tarehe 18 Des... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More