CCM YAFUNGA KAMPENI MONDULI KWA KISHINDO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CCM YAFUNGA KAMPENI MONDULI KWA KISHINDO

Chama cha Mapinduzi(CCM) leo kimehitimisha kampeni zake za ubunge jimbo la Monduli kwa aina yake kutokana na wapambanaji wake kujipanga vyema katika kubwaga sera wakimnadi mgombea wa chama hicho Julius Kalanga.

Kampeni hizo zimefurika mamia ya wakazi wa jimbo hilo katika eneo la Mto wa Mbu na zimefungwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara Rodrick Mpogoro na mgeni mashuhuri Selemani Jafo ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI).

Timu ya wapambanaji wengine iliyokuwa kwenye kampeni hizo kwa siku zote iliongozwa na William Ole Nasha, pamoja na timu ya wabunge mahiri Joseph Msukuma, Sixtus Mapunda, Catherine Magige, Ester Mahawe, Venanse Mwamoto, Dk. Kiluswa, Mariam Ditopile, Matha Mlata, Dk. Godwin Mollel, Anna Lupembe, Edwin Sanda, Godluck Mlinga, Jitu Son, Fratei Massey, na viongozi wengine wa Jumuiya zote za CCM Taifa.

Wapambanaji hao wamewaomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua mgombea huyo kuwa Mbunge wao ili aweze kutatua vyema kero zinazowakabili kwa kushirikiana vyema na wabunge wengine huku wakiahidi kumsaidia kuwasilisha bungeni kero za watu wa Monduli ili zitatuliwe na serikali.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara Rodrick Mpogoro akiwa na viongozi wengine katika ufungaji wa kampeni za ubunge jimbo la Monduli.

Mbunge wa Kisarawe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akizungumza katika ufungaji wa kampeni za ubunge jimbo la Monduli.

Wananchi waliohudhuria kampeni za ubunge za CCM jimbo la Monduli
Wananchi waliohudhuria kampeni za ubunge za CCM jimbo la Monduli

Wananchi waliohudhuria kampeni za ubunge za CCM jimbo la Monduli


Source: Issa MichuziRead More