CCM YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUTELEZA ILANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CCM YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUTELEZA ILANI

Na Tiganya VincentHALMASHAURI kuu ya CCM Mkoa wa Tabora imeipongeza Serikali ya Awamu ya tano kutokana na kutekeleza kwa vitendo Ilani yake ya miaka mitano tangu ulipofanyika uchaguzi Mkuu uliopita mwaka 2015 hadi sasa.
Pongezi hizo zimetolewa jana kwenye kikao maalumu cha wajumbe wa Halmashauri hiyo iliyokutana kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kutoka serikali ya Mkoa wa Tabora.
Wajumbe hao walisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dokta John Pombe Magufuli iliahidi miradi mbalimbali kwa wakazi wa Mkoa huo ikiwemo ya maji, afya, barabara na kilimo ambapo utekelezaji wake unaonekana kwa macho.
Waliitaja miradi ambayo utekelezaji wake umeanza na unaendelea kwa kasi mkoani humo kuwa ni wa maji kutoka ziwa Victoria kwa ajili ya wakazi wa Wilaya za Nzega, Tabora na Igunga.
Miradi mingine ni ujenzi wa barabara za kiwango cha lami kuunganisha Mkoa huo na mikoa jirani ambapo ujenzi unaendelea.
Katika hatua nyingine wajumbe hao wamezitaka Halmashauri  za wilaya mkoani humo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More