CCM YASHINDA UDIWANI KATA YA MAWENZI,KILIMANJARO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CCM YASHINDA UDIWANI KATA YA MAWENZI,KILIMANJARO

Na Dixon Busagaga ,Moshi.

MGOMBEA udiwani katika kata ya Mawenzi ,manispaa ya Moshi ,Apaikunda Naburi (CCM) amefanikiwa kushinda nafasi hiyo akiwashinda wagombea wengine baada ya kupata kura 400 sawa na asilimia 70.3 kati ya kura 569 zilizopigwa.

Naburi aliyekuwa diwani wa kata ya Mawenzi katika kipindi cha mwaka 2010-2015 kabla ya kushindwa na aliyekuwa Diwani wa kata hiyo ,Hawa Mushi aliyefariki dunia hivi karibuni baada ya kuugua ghafla.Mgombea huyo amefanikiwa kurejea kwenye nafasi hiyo kwa kuwashinda Afrikana Mlay wa Chadema na na Isaac Kereti wa SAU waliokuwa wakiwania kiti hicho.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi msimamizi wa uchaguzi , Erasmo Silayo alimtangaza Naburi kuwa mshindi halali wa kiti hicho huku akitaja kura za mgombea aliyefuatia kuwa ni Afrikana Mlay (Chadema) aliyepata kura 163 huku mgombea Isack Kireti (SAU) akiambulia kura 2.

.Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi,Naburi amewashukuru wapiga kura katika kata hio huku akiwaahidi ushirikiano katika... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More