CCM ZANZIBAR YAVUNJA NGOME YA UKAWA YAVUNA VIGOGO 7 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CCM ZANZIBAR YAVUNJA NGOME YA UKAWA YAVUNA VIGOGO 7

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesambaratisha ngome ya uliokuwa Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA) kwa kung’oa vigogo saba na wanachama wengine wa Chama kilichokuwa mshirika wa umoja huo.
Vigogo hao waliong’oka kutoka Chama Cha ukombozi wa umma(CHAUMMA) ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama Taifa wa Chama hicho Ndugu Salma Mohamed Juma, Mwenyekiti wa Vijana wa Wilaya ya Mjini wa Chama hicho Ndugu Salamuu Abdalla Juma.
Wengine ni Katibu wa Vijana Wilaya ya Mjini ndugu  Mwanabaraka Ali Mohamed, Mjumbe wa chama hicho Wilaya ya Mjini Shadya Juma Khamis, Mjumbe wa Chama hicho  Mkoa wa Magharibi Mariam Peter John  pamoja na Mjumbe wa  ngazi ya wilaya ya Mjini Raya Ali Masoud.
Viongozi hao wa CHAUMA leo wamejiunga rasmi na CCM na kupewa kadi za Chama Cha Mapinduzi na Umoja wa Wanawake wa Tanzania(UWT) hafla iliyofanyika katika Afisiu ya UWT Wilaya ya Dimani Unguja.
Akizungumza mara baada ya kujiunga na CCM, aliyekuwa Mwenyekiti wa Wanawake... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More