CEO WA DAWASA AHAIDI KUPELEKA HUDUMA YA MAJI BONYOKWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CEO WA DAWASA AHAIDI KUPELEKA HUDUMA YA MAJI BONYOKWA

OFISA mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka  Dar es Salaam  (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja ametoa ahadi ya kupeleka maji Bonyokwa  wakati wa ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa.
Prof. Mbarawa amefanya  ziara ya kusikiliza kero za wananchi kuhusiana na huduma ya Maji katika eneo hilo. 
Mhandisi Luhemeja ameeleza kuwa eneo hilo limekosa huduma ya Maji kwa muda mrefu kutokana na kukosa chanzo cha Maji cha Karibu na hivyo DAWASA imeamua kulaza bomba kubwa litakalo chukua Maji kutoka mtambo wa uzalishaji Maji wa Ruvu juu ili kuhudumia wakazi wa eneo hilo.
“Sisi DAWASA tutaleta huduma ya Maji hapa Bonyokwa kwa kuwa ni muda mrefu mmeteseka na tatizo kubwa la eneo hili ni kukosa chanzo cha Maji cha kuhudumia hapa kutokana na jiografia yake ila sasa tumeamua kutoa Maji kutoka mtambo wa Ruvu juu na kuyaleta hapa, tayari pia baadhi ya vifaa vimefika hapa na kuanzia Siku ya Jumatatu tutaanza kazi rasmi ya kulaza mabomba hivyo wananchi mjitokeze kwa ajira ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More