CHADEMA WADAI KATIBA MPYA UCHAGUZI HURU - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CHADEMA WADAI KATIBA MPYA UCHAGUZI HURU

Wananchi wakiwasikiliza viongozi wa Chadema walioongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kwenye Kampeni za Ubunge Jimbo la Monduli Jana picha na mahmoud Ahmad Monduli.
Na Ahmed Mahmoud Arusha.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa wamesema baada ya kumalizika kwa chaguzi ndogo nchini wataibuka na ajenda ya kudai haki na uhuru sanjari na mabadiliko ya katiba mpya ambayo italinda Amani na uhuru wa watanzania.
Wamesema uhuru na haki unavunjwa licha ya Katiba ya nchi kufafanua kwa kina kuhusu mambo hayo kwani ukiona katiba inavunjwa haki haipo hivyo wanaonana jambo la msingi ni katiba mpya ambayo itakuwa ajenda yao kuu kuanzia sasa..
Wametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 13, 2018 katika mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Monduli, Yonas Laizer ambapo wamesema kuwa ili nchi iwe na amani ya kweli lazima Haki na Uhuru viwepo kinyume chake ni kuwepo na uvunjwaji wa wazi wa katib... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More