Chama cha Kifaidhina chashinda Uchaguzi Ugiriki - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Chama cha Kifaidhina chashinda Uchaguzi Ugiriki

Kiongozi wa upinzani wa chama cha kihafidhina nchini Ugiriki Kyriakos Mitsotakis ameapishwa baada ya kushinda uchaguzi wa bunge uliofanyika Jumapili.


Waziri Mkuu Alexis Tsipras anayeondoka amekubali kushindwa, amesema chama chake kimekubali uamuzi wa wapiga kura. Tsipras aliiongoza Ugiriki kwa miaka minne wakati wa mzozo mkubwa wa kifedha.


Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Ugiriki, chama cha New Democracy cha mwanasiasa Mitsotakis kimepata asilimia 39.8 ya kura huku chama cha mrengo wa shoto cha Syriza cha Waziri Mkuu Tsipras kikiwa kimepata asilimia 31.5.


Mitsotakis ameahidi kupunguza kiwango cha kodi, kuvutia uwekezaji na kubuni nafasi zaidi za kazi mara atakapoanza kuutumikia wadhifa wake mpya wa uwaziri mkuu.


Kwenye uchaguzi huo, chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Golden Dawn, ambacho kiliundwa na wanazi mamboleo na kilichokuwa cha tatu kwa ukubwa katika bunge la Ugiriki kimeshindwa kurejea bungeni.


Matokeo ya uchaguzi huo yameonesha kuwa wapiga kura wa Ugiriki w... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More