CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAENDELEA KUKEMEA UMIMI, UBINAFSI NA MAKUNDI NDANI YA CCM ILI KUIMARISHA UIMARA, UMOJA NA UMADHUBUTI WA CCM - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAENDELEA KUKEMEA UMIMI, UBINAFSI NA MAKUNDI NDANI YA CCM ILI KUIMARISHA UIMARA, UMOJA NA UMADHUBUTI WA CCM

Katika kikao cha Halmashauri Kuu Maalumu ya CCM Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinakemea vikali umimi, ubinafsi na makundi ndani ya CCM ili kuimarisha uimara, umoja na umadhubuti wa CCM.
Akieleza kwa kina suala hilo Ndg. Polepole amesema umimi, ubinafsi na makundi ni kinyume na Katiba, Kanuni na Taratibu nzuri za CCM na kuwa ndani ya CCM Makundi hayana nafasi hususani katika kipindi hiki ambacho muelekeo wa CCM ni kushughulika na utatuzi wa shida za wananchi.
Aidha Ndg. Polepole amewataka wanaCCM na Viongozi kuwa wamoja, kushikamana, kushirikiana na kupendana ili CCM izidi kuwa imara na iendelee kuwa hudumia wananchi ipasavyo.
“Chama hiki nikikubwa kuliko mtu mmoja, hatuwezi tukaruhusu tabia za hovyo ambazo tumezikataza, tabia za makundi, hata Ndg. Magufuli Mwenyekiti wetu mpendwa hapendi makundi kwa sababu makundi hayatujengi na yanadhoofisha umoja wa  Chama chetu” amesema Ndg. Polepole
Wakati... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More