chama cha wataalamu waliobobea kupambana na ufisadi wakutana kujadili njia za kumaliza ufisadi - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

chama cha wataalamu waliobobea kupambana na ufisadi wakutana kujadili njia za kumaliza ufisadi

Na Woinde Shizza,Michuzi TV-Arusha

CHAMA cha wataalamu waliobobea katika kupambana na Ufisadi duniani (ACFE)kimejipanga kuanza kutumia teknolojia za kisasa katika kubaini na kuchunguza uhalifu huo unaoonekana kushika kazi katika nchi mbalimbali duniani.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo katika mkutano mkuu wa chama hicho,unaofanyika tawi la Tanzania, jijini Arusha ,Rais wa ACFE ,Emanuel Johanness alisema lengo kubwa la mkutano huo ni kuangalia mapambano ya ufisadi katika siku za usoni kutokana na aina ya ufisadi kuhamia kwenye kiteknolojia zaidi.

Alisema taarifa yao ya mwaka jana 2018 imeonyesha kuwa katika kesi 2690 za ufisadi zilizoripotiwa kutoka nchi 125 duniani katika sekta mbalimbali 23, imeonyesha kuwa kiasi cha dolla za kimarekani billion 7 zimepotea kutokana na ufisadi unaofanyika kwenye taasisi za umma ,makampuni na sekta binafsi.

Alisema kuwa njia sahihi inayotumika kwa sasa kubaini ufisadi ni pamoja na kupewa taarifa za siri kutoka kwa wananchi wazalendo ,amba... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More