Videos by BBC Swahili | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 Videos by BBC Swahili

MV NYERERE:  Fundi mkuu wa kivuko kilichozama Tanzania azungumza na BBC

Channel : BBC Swahili

MV Nyerere: “Nilijipata niko chini nikama mtu kapigwa ngwala ... Haya mafiga unayoona hapa yanaashiria kuwa jamaa zangu walikuwa na msiba tayari. Picha yangu unayoiona hapo pembeni ilikuwa imewekwa nje Kwa sababu ya kuongoza mazishi” Augustine Cherehani Fundi mkuu wa Mv Nyerere alipozuzungumza na Eagan Sallah .Burundi yatuhumu  Pierre-Celestin Ndikumana kwa njama ya kumuua rais Pierre Nkurunziza

Channel : BBC Swahili

Serikali ya Burundi imemtuhumu mwanasiasa maarufu wa upinzani kwa kupanga njama ya kumuuarais wa nchi hiyo. Idara ya Polisi nchini humo inasema Mbunge Pierre-Celestin Ndikumana kutoka Muungano wa mpinzani Mkuu Agaton Rwasa, alipanga njama ya kumuua rais Pierre Nkurunziza, pamoja na maafisa wengine wa vyeo vya juu wakiwemo wabunge wawili. Hata hivyo, Mbunge Ndikumana ameyakana madai hayo na kusema ni njia ya serikali ya kutaka kuukandamiza upinzani na kuzua hali ya hofu nchini Burundi. Kutoka Bujumbura , Mwandishi wetu Ramadhani Kibuga ana taarifa zaidi.Mbwa anayemlea Simba

Channel : BBC Swahili

Baada ya kutelekezwa na mama yake mzazi waka wa 2014Kituo kimoja cha kuhifadhia wanyama pori nchini Sri Lanka kililazimika kuchukua hatua.Kituo kimoja cha kuhifadhia wanyama pori nchini Sri Lanka kililazimika kuchukua hatua.Walimtafuta mbwa jike aliyekuwa amejifungua na wakampa mwana simba huyuMV Nyerere: Je kuna mabadiliko na mafunzo yoyote mwezi mmoja baadaye ?

Channel : BBC Swahili

Mwezi mmoja sasa tangu kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere, ziwa Victoria, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, ajali ambayo ilisababisha vifo vya watu zaidi ya 220. Lakini hali ya usafiri na usalama wa majini imebadilika kwa namna yoyote tangu kutokea kwa ajali hii? MV Saba Saba ni moja ya kivuko kinachofanya shughuli yake kutoka Ukerewe hadi katika kisiwa cha Ukara, kama ilivyokua kwa MV Nyerere iliyozama mwezi mmoja tuu uliopita.Mo Dewji: Kamanda Siro azungumza

Channel : BBC Swahili

Inspekta mkuu wa polisi nchini Tanzania,Simon Sirro, amesema uchunguzi umebaini kuwa gari lililotumiwa kumteka nyara mfanyabiashara tajiri Mohammed Mo Dewji lilitoka nchi jirani. Picha : Eagan SallahBBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 18.10.2018

Channel : BBC Swahili

Na Salim Kikeke & Dayo YusufMsafiri Zawose: Mwanamuziki Mtanzania anayetetea muziki wa kitamaduni

Channel : BBC Swahili

Muziki wa asili nchini Tanzania haufurukuti mbele ya muziki wa kizazi kipya ambao unapatiwa muda wa kutosha katika vyombo vya habari na hata wasanii wake kupata nafasi ya kushiriki matamasha makubwa nje na ndani ya Tanzania Msafiri Zawose ambaye ni msanii wa muziki wa Asili toka Tanzania amejijengea jina kubwa katika mataifa ya bara Ulaya na Marekani kwa aina ya muziki anao ufanya Msafiri ambaye hutumia ala za asili kama vile zeze na marimba katika Muziki wake ana amini kwamba ipo siku Muziki huu wa asili utapata heshima nchini Tanzania na kwingineko barani Afrika Video: Eagan SallaBBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 17.10.2018

Channel : BBC Swahili

Na Salim Kikeke & Dayo YusufBBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 16.10.2018H

Channel : BBC Swahili

Na Salim Kikeke & Dayo YusufBBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 15.10.2018

Channel : BBC Swahili

Na Salim Kikeke & Dayo YusufBBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 12.10.2018

Channel : BBC Swahili

Na Zuhura Yunus & Zawadi MachibyaWatu 55 wafariki katika ajali ya basi Kenya wakielekea Kisumu

Channel : BBC Swahili

Watu 55 wamefariki dunia nchini Kenya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali kwenye barabara kuu ya Nairobi-Kisumu. Walioshuhudia wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea leo mwendo wa saa kumi na moja alfajiri. Ajali hiyo mbaya ilitokea katika eneo la Fort Ternan Kaunti ya Kericho.Wenye matatizo ya kiakili, wanafungwa minyororo Ghana

Channel : BBC Swahili

Nchini Ghana kuna madaktari wa afya ya kiakili 25 pekee wanaostahili kuhudumia takriban watu milioni 30. Uhaba huu wa madaktari umesababisha jamaa za watu wenye matatizo ya kiakili, kuwategemea viongozi wa kidini. Hata hivyo viongozi hawa hawana ujuzi wa kitabibu na hivyo wanaishia kuwafunga minyororo ilikuwadhibiti wanaokisiwa kuwa ni 'wenda wazimu'. Serikali iliharamisha tabia ya kuwafunga minyororo mwaka uliopita hata hivyo uchunguzi wa BBC umebaini kuwa sasa viongozi hao wa kidini wamewajengea vyumba vidogo kuwadhibiti. Tazama ripoti hii kutoka Ghana, ya Sulley LansahBBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 11.10.2018

Channel : BBC Swahili

Na Zuhura Yunus na Beryl WambaniMalkia Nanny: Mwanamke aliyetoroka utumwa Jamaica na kuwa malkia

Channel : BBC Swahili

Nanny alizaliwa karibu mwaka 1686 katika jamii ya Asante katika sehemu ambayo sasa inafahamika kama Ghana, Afrika Magharibi. Baada ya kusafirishwa hadi Jamaica kama mtumwa, alitoroka na kuwa kiongozi wa kundi la watumwa huru na anafahamika zaidi kama Queen Nanny. Hii ni sehemu ya mfululizo wa makala ya BBC kuhusu wanawake wa Afrika waliyobadilisha dunia.BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 10.10.2018

Channel : BBC Swahili

Na Zuhura Yunus & Beryl WambaniMbwana Samatta:

Channel : BBC Swahili

Mtanzania Mbwana Ally Samatta amefanikiwa sana akicheza soka Ulaya katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, lakini hakuwa hivi tangu zamani. Alianzaje na nini kilimpa msukumo wa kuendelea kujiboresha? Alizungumza na mwandishi wa BBC Salim Kikeke.Channel : BBC Swahili

Saratani ya matiti inapozungumziwa, moja kwa moja kinachowaingia fikirani watu wengi huwa ni wanawake. Lakini wajua kuwa ugonjwa huu pia huwaathiri wanaume ? Moses Musonga, 67, ni mmoja wa wanaume wanaougua saratani ya matiti. Aligunduliwa kuwa na ugonjwa huu mwaka wa 2013 alipofika hospitalini kupata matibabu kutokana na uvimbe uliotokea kwenye titi lake la kulia.BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 09.10.2018

Channel : BBC Swahili

Na Zuhura Yunus & Beryl WambaniKenya: Je utumiaji wa tarakilishi utawapa wanawake wafungwa fursa mpya?

Channel : BBC Swahili

Idadi ya wafungwa ambao wanaorejea kwenye tabia za uhalifu ni vigumu kuonekana katika nchi kadhaa barani Afrika, lakini nchini Kenya takwimu zinaonesha kwamba asilimia 80% ya wafungwa hurejea magerezani. Mjasiriamali mmoja nchini Kenya anabadilisha mtindo huo kwa kutumia teknolojia. Wafungwa katika gereza moja kuu la wanawake wanapata mafunzo ya kompyuta. Taarifa ya mwandishi wa BBC DHRUTI SHAH inawasilishwa na Nasteha Mohammed.