Videos by Bongo 5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 Videos by Bongo 5

Vunja Mbavu: Kilichomtokea Dogo Pepe baada ya kulikoroga!

Channel : Bongo 5Vunja Mbavu: Dogo Pepe ashindwa kupewa chake kisa Kingereza!

Channel : Bongo 5

Umewahi kukosa huduma kisa lugha ya Kingereza, Dogo Pepe amekutwa na janga hilo.Dogo Pepe abambwa na mke wake akiomba namba kwa mchepuko

Channel : Bongo 5

Mchekeshaji Dogo Pepe amejikuta matatani baada ya kushtukiwa akiomba namba za mchepuko huku mke wak akiwa anamuona.TECNO waja na VIMBA SEASON: Kila mteja atashinda Simu, Jagi, Pasi n.k

Channel : Bongo 5

Kampuni ya Tecno Tanzania imekuja na Ofa ya Vimba Season ambayo itamuwezesha mteja yeyote atakayenunua simu ya Tecno kujishindia zawadi kemkem. Kwenye msimu huu wa Vimba Season watumiaji watakaonunua simu za Tecno wataingia moja kwa moja kwenye droo na kushiriki na uzuri ni kwamba hakuna mtu anayekosa zawadi.Hivi ndivyo Ridhiwani Kikwete alivyomuaga Babu yake makaburini.

Channel : Bongo 5

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ameweza kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha babu yake mzee Rashidi anahifadhiwa vizuri katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar Es Salaam,lakini pia mazishi haya yameweza kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo rais mstaafu Ally Hassani Mwinyi na wAZIRI Mkuu Mheshimiwa Kassimu Majaliwa.HATARI: huu ndio ugonjwa unaomsumbua Ommy Dimpoz/Wasanii waonywa na Daktari

Channel : Bongo 5

Ni mwezi sasa umepita tangu msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz atangaze hadharani kuwa afya yake haipo sawa baada ya kufanyiwa matibabu nchini Kenya bila mafanikio na kushauriwa kwenda nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Ingawaje Ommy Dimpoz hakuweka wazi ni ugonjwa gani hasa unaomsumbua lakini kwenye mahojiano yake na mchambuzi wa soka Tanzania, Eddo Kumwembe alinukuliwa akisema amefanyiwa upasuaji wa Koromeo. Akielezea kwenye mahojiano hayo Ommy Dimpoz alisema kuwa  awali alianza kuona dalili za kukaukiwa koo na baadaye alishindwa kabisa kumeza chakula wala kitu chochote mdomoni. Je,dalili hizo huenda zikawa za ugonjwa gani? Bongo5 imemtafuta mtalaamu wa magonjwa ya kinywa na meno, Dkt. Onesmo Ezekiel Kapugi kutoka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (BOMBO) ambaye yeye ameleeza kuwa dalili hizo za kushindwa kumeza chakula kitaalamu inaitwa Dysphagia na ni dalili ya magonjwa ya vinywa. Dkt. Kapugi amesema dalili hizo mara nyingi zinaweza kupelekea magomjwa ya Parkinson ambayo yanasababishwa na neva za fahamu kushindwa kufanya kazi vizuri ikiwemo kusinyaa kwa koromeo. Akitaja chanzo hasa cha magonjwa kama hayo kwa wasanii amesema kuwa mara nyingi wasanii wanapoimba kwenye koromeo kuna kitu kinaitwa Vocal Cords na kama msanii ataimba kwa muda mrefu huwa vocal cords zinavimba na baadaye kupelekea maumivu kwenye koromeo na kushindwa kula wala kumeza kitu chochote.Ridhiwani Kikwete aeleza chanzo cha kifo cha Babu yake na ratiba ya mazishi

Channel : Bongo 5

Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Bi. Salma Kikwete amefiwa na baba yake mzazi mzee Rashid Mkwachu usiku wa kuamkia leo.Mzee Pinda, Mbowe, Waziri Majaliwa wakimpa pole KIKWETE kwa kufiwa

Channel : Bongo 5

Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Bi. Salma Kikwete amefiwa na baba yake mzazi mzee Rashid Mkwachu usiku wa kuamkia leo. kufuatia kifo hicho hicho viongozi mbalimbali wamejitokeza nyumbani kwa Kikwete wakimpa poleBREAKING: Wema aachiwa huru na Mahakama/Wakili wake afunguka

Channel : Bongo 5

Wakili wa Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu, Alberto Msando amesema kuwa tayari mteja wake ameshalipa faini ya milioni 2 na ameshakuwa mtu huru. Hii ni baada ya asubuhi ya leo Mahakama ya Mkazi Kisutu kumhukumu msanii huyo kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya milioni 2 kwa kukutwa na makosa mawili ya kutumia na kuhifadhi madawa ya kulevya aina ya bangi nyumbani kwake.WEMA ahukumiwa jela mwaka mmoja/STEVE NYERERE aishukuru Mahakama

Channel : Bongo 5

Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya milioni 2 baada ya kukutwa na makosa mawili ya kutumia na kuhifadhi dawa za kulevya aina ya Bangi nyumbani kwake. kufuatia hukumu hiyo Steve Nyerere ameishukuru mahakama kwa maamuzi hayoPETIMAN afunguka baada ya WEMA kuhukumiwa mwaka mmoja jela

Channel : Bongo 5

Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya milioni 2 baada ya kukutwa na makosa mawili ya kutumia na kuhifadhi dawa za kulevya aina ya Bangi nyumbani kwake. Rafiki yake wa Karibu Petiman afungukaWeusi wafanya kweli uzinduzi wa vipindi vya Dstv

Channel : Bongo 5

Wasanii wa muziki wa hip hop Bongo kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili, Joh Makini na G Nako wamekonga nyoyo za mashabiki usiku wa leo wakati wa uzinduzi wa vipindi vya Harusi yetu na Huba vinavyorushwa na Kampuni ya DSTVQ Chief: Nimefanyiwa counselling/ Sitaki mpenzi/ Media zinisamehe / na swali swala 5

Channel : Bongo 5

Bongo5 imefanya jitihada za kumtafuta msanii wa muziki, Q Chief baaada ya kuwa kimya kwa miezi miwili toka atangaze kuaachana na muziki. Muimbaji huyo amesema kwa sasa amefanyiwa canceling na amerudi upywa kwenye muziki huyo akiahidi kutowaangusha tena Watanzania.Kingereza cha Shilole: Waweze Ku Sapu klaibu/ My husband she

Channel : Bongo 5

Shilole bado anaendelea kujifunza kuongea kiingereza, wiki hii alibambwa na Bongo5 wakati anatamka neno subscribe ambapo alirudia zaidi ya mara kumi lakini akashindwa kulitamka.G Nako: Milioni 5 ni tozo kubwa /

Channel : Bongo 5

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo kutoka kundi la Weusi, G Nako ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya wa Nyatu Nyatu amesema kuwa tozo ya milioni tano ni kiasi kikubwa sana huku akizungumzia 'style' ya Kikuku kuwa imekuwa ikitumika hata kwa watu jamii ya wamasai.Irene Paul awataka watu kuheshimu hisia za Muna Love

Channel : Bongo 5

Muigizaji wa filamu nchini, Irene Paul amesema kuwa nilazima watu waheshimu hisia za mwanadada Muna Love kama mzamzi na kamwe hastaili kulaumiwa hii inakuja baada ya mfiwa huyo kuzungumza na vyombo vya habari hapo jana zikiwa zimepita siku chache tu toka kumzika mwanae Patrick.Dstv yazindua rasmi vipindi vyake pendwa vya Harusi yetu na Huba

Channel : Bongo 5

Mkuu wa Channeli ya Maisha Magic Bongo inayopatikana kwenye king'amuzi cha Dstv 160, Barbara Kambogi amezindua rasmi vipindi viwili vya Harusi yetu na Huba vinavyopatikana kwenye kwenye kampuni hiyo ikiwa ni msimu wake wa tatu.Meneja wa Q Chief: Q Chief hakuwa na afya nzuri/ Sikupenda niandike RIP

Channel : Bongo 5

Kampuni ya Alfa Chain International inayomsimamia muimbaji Abubakar Katwila aka Q Chief imeeleza kwanini iliamua kufanya kazi za msanii huyo muda mchache baada ya kutangaza kwamba anaachana na masuala ya muziki. Meneja wa kampuni hiyo aitwae, Warren Bright amesema afya ya Q Chief pamoja na thamani yake katika muziki wa BongoFleva ndio kitu ambacho kimsukuma kusafiri kutoka Marekani hadi Tanzania ili kumuokoa.Joh Makini: Nachukulia kama

Channel : Bongo 5

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo kutoka kundi la Weusi, Joh Makini amesema kuwa nyimbo yao mpya ya Mdundiko inakwenda vizuri huku akiomba kuwe na majadiliano baina ya wasanii na Sanerakili kuhusiana na ada mpya zinazotozwa na BASATA.Tazama Joti alivyowavunja mbavu watu uzinduzi wa vipindi vya Dstv

Channel : Bongo 5

Mchekeshaji kutoka Kundi la Orijino Komedi, Lucas Mhuvile ‘Joti’ hapo jana usiku amenogesha uzinduzi wa vipindi vya Kampuni ya Dstv baada ya kuwavunja mbavu kwa vicheko watu wengi waliyohudhuria ghafla hiyo.