CHANZO KIMOJAWAPO CHA AJALI ZA BARABARANI NI UCHOVU WA MADEREVA -DKT. MPOKI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CHANZO KIMOJAWAPO CHA AJALI ZA BARABARANI NI UCHOVU WA MADEREVA -DKT. MPOKI

Na WAMJW, Dar es Salaam.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa moja ya sababu za ajali barabarani, ni uchovu wa madereva.

Dkt. Mpoki ameyasema leo Novemba 13,2018 wakati wa kufungua mafunzo ya watoa huduma za tiba, uokoaji na usafirishaji wa majeruhi wa ajali na wagonjwa wenye dharura mbalimbali nje ya Hospitali nchini.

Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo, Dkt. Mpoki amelitaka jeshi la Polisi nchini kuangalia namna ya kuweka utaratibu wa madereva kubadilishana kwani suala la uchovu linachangia kwa kiasi kikubwa ajali za barabarani.Aidha,akitolea mfano suala la uchovu, dereva kutoka Mwanza au Bukoba kwenda Dar es Salaam, basi ashuke Singida ili aingie dereva mwingine kumalizia safari na hiyo itasaidia kuepusha ajali.

“Tumemuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi atusaidie kama mchango wa Polisi katika kupunguza ajali kwa kuhakikisha kwamba wanaweka utaratibu wa madereva wanaendesha kwa muda maalum. Kuliko il... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More