Chemical Amwaga Povu Zito Baada Ya Kuvaa Gauni - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Chemical Amwaga Povu Zito Baada Ya Kuvaa Gauni

Msanii wa muziki wa hip hop nchini Claudia Lubao maarufu Kama Chemical amejikuta anawatolea povu zito watu ambao wamediss baada ya kuonekana akiwa amevaa gauni.


Chemical amejizolea umaarufu kwenye muziki wa hi hop Kama mwanadada mgumu ambaye mara amekuwa akitinga mavazi ya kiume pekee lakini Siku chache zilizopita Chemical aliposti picha akiwa amevaa gauni.Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers baada ya sakata hilo,Chemical aliyekuwa amevaa kigauni hicho na kutokelezea kwenye ukurasa wake wa Instagram alisema kuwa, haoni kama ni tatizo kuvaa nguo hizo japokuwa wengi wameshazoea kumuona akiwa katika mavazi ya kiume mara kwa mara.Wengi walishazoea kuniona na nguo za kiume muda wote, wakati ninavaa lile gauni nilijua tu kwamba wataiongelea kwa sababu kuongea ni kawaida yao, kwa hiyo hawaniumizi kichwa, ninachojua mimi ni mtoto wa kike hivyo nina uamuzi wa kuvaa nguo yoyote ninayoona kwangu inafaa ilimradi tu nisivunje maadili yetu ya Kitanzania“. 


The post Chemical Amw... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More