Chid benz Akanusha Kuwa na Bifu na Harmonize, Aongelea Mahusiano Yake na Wasanii Wenzake. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Chid benz Akanusha Kuwa na Bifu na Harmonize, Aongelea Mahusiano Yake na Wasanii Wenzake.

Msanii wa muziki wa siku nyingi Chid benz amefunguka na kuongelea mahusiano yake na msanii anaefanya vizuri sasa hivi katika sanaa ya bongo fleva Harmonize na kusema kuwa hakuna tatizo kubwa kati yake na Harmonize .Na hata kama litakuwepo , anaogopa hata watu watamshangaa na kumuona kuwa yeye ana wivu.


Hakuna tatizo kati yangu na harmonize na sdhani kama kutakuwa na tatzio lolote,na kama kutakuwa na tatizo kati yangu na harmonize lazima watu watanishangaa.kama kutakuwa na ugomvi  kati yangu na yeye basi ujue kuwa watu wanaweza hata kusema kuwa mimi nina mawivu yangu tu.


Lakini pia ninachoshukuru  ni kwamba karibia wasanii wote  wananipa respect sana mimi,mimi sinaga ubaguzi na mtu yoyote , kwa sababu mimi naongea na kila mtu, na nina heshimu kila mtu pia. 


Lakini pia Chid benz amefunguka na kusema kuwa yeye ni moja ya wasanii wasiopenda unafiki hata siku moja na ndio maana kila mtu anapofanya kosa huwa anataka kuonana na mtu husika na kumwambia moja kwa moja na wala hana kujificha ... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More