CHIRWA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO AZAM FC AKICHEZA MECHI YA KWANZA TU TIMU IKISHNDA 2-0 DHIDI YA U23 YA TANZANIA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CHIRWA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO AZAM FC AKICHEZA MECHI YA KWANZA TU TIMU IKISHNDA 2-0 DHIDI YA U23 YA TANZANIA

Na Saada Salmin, DAR ES SALAAM
AKICHEZA mechi yake ya kwanza tokea asajiliwe na Azam FC, mshambuliaji Obrey Chirwa, amefungua akaunti ya mabao kwa kufunga moja wakati timu hiyo ikiilaza timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23 (Ngorongoro Heroes) mabao 2-0.
Mchezo huo wa kirafiki umefanyika Uwanja wa Azam Complex usiku huu, Ngorongoro Heroes ikiutumia kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya vijana wenzao wa Burundi.
Azam FC ilipata bao la uongozi dakika ya 12 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na winga Enock Atta, ambaye kwenye mchezo huo alicheza kama kiungo mchezeshaji, penalti hiyo ilipatikana baada ya Ramadhan Singano ‘Messi’, kuangushwa ndani ya eneo la hatari.
Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Mzambia Obrey Chirwa (kulia) akimtoka beki wa U23 ya Tanzania leo 
Beki na Nahodha wa U23 ya Tanzania, Abdallah Shaibu 'Ninja'  akiwa chini kuokoa dhidi ya mshambuliaji Mzimbabwe wa Azam FC, Donald Ngoma
Nahodha Abdallah Shaibu 'Ninja' (kulia) akimdhibiti mshambul... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More