CHUO CHA MAJI WAHIMIZA VIJANA WALIOSOMA MASOMO YA SAYANSI KUJIUNGA KATIKA CHUO HICHO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CHUO CHA MAJI WAHIMIZA VIJANA WALIOSOMA MASOMO YA SAYANSI KUJIUNGA KATIKA CHUO HICHO

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.
CHUO cha Maji kimesema changamoto kubwa iliyopo katika sekta ya maji nchini ni uhaba wa watalaamu ,hivyo jukumu la chuo hicho kuendelea kuandaa watalaamu  ambao watakuwa watakuwa wamebobea katika eneo sekta ya maji ili kuondoa changamoto hiyo.
Katika kuhakikisha changamoto hiyo inamalizwa Chuo hicho kimetoa rai kwa Watanzania na hasa vijana ambao wamesoma masomo ya sayansi na kufaulu vizuri wakajiunga na chuo hicho kwani tayari wameanza kupokea maombi ya wanaotaka kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo unaonza 2018.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam katika Maonyesho ya 13 ya Vyuo Vikuu ya Elimu ya Juu Tanzania (TCU) na Ofisa Masoko wa Chuo cha Maji Ghanima Chanzi.Amesema kuwa chuo hicho kimedhamiria kuondoa changamoto hiyo kuwa kuhakikisha wanapatikana wahitimu waliohitimu masomo yanayotolewa na chuo hicho kwa ajili ya kulitumikia taifa kaika eneo la sekta ya maji.
"Wapo watalaam ambao wanatoa huduma katika eneo hilo lakini bado kuna changamoto ku... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More