CHUO CHA UANDISHI WA HABARI DSJ WAPATA RAIS MPYA, AAPISHWA RASMI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CHUO CHA UANDISHI WA HABARI DSJ WAPATA RAIS MPYA, AAPISHWA RASMI

Na Khadija Seif,globu ya jamii
RAIS mpya wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam(DSJ) Esther Amandus ameapishwa rasmi huku akitumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa wote walioshiriki uchaguzi huo.
Sherehe za kuapishwa kwa Rais huyo pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali umefanyika leo chuoni hapo.Pia wanafunzi wengine waliopo na wale waliowasoma chuoni hapo walishiriki tukio hilo.
Akizungumza chuoni hapo Amandus ametoa shukrani kwa kila mmoja aliyeshiriki kwenye uchaguzi kwani wote walifanya uchaguzi wa haki na demokrasia .

Amesema anatarajia kufanya kazi na wanafunzi wote wa DSJ katika kuzisikiliza shida ,kero na mahitaji yao ili kutetea maslahi ya chuoni hicho.

Pia ameshukuru uongozi chuoni hapo na kuwaomba kushirikiana nao bega kwa bega katika kukiletea maendeleo chuo .
Amesisitiza chuo cha DSJ kimetoa waandishi mahiri ambao wako kwenye tasnia ya habari nchini akiwemo Salum kikeke,Charles Hillary na wengine wengi ambao wameleta mapinduzi kwenye habari na kuwa mifano ya kuigwa... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More