CLEMENT SANGA AVULIWA UENYEKITI BODI WA LIGI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CLEMENT SANGA AVULIWA UENYEKITI BODI WA LIGI

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekubaliana na mapendekezo ya Kamati ya Sheria na Katiba ya kumsimamisha, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Clement Sanga baada ya kukosa sifa za Uenyekiti wa Bodi hiyo. 
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam, Rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia amesema kwamba hatua imefuatia Mkutano wa Juni 10 wa wanachama wa Yanga kusema bado unamtambua Yussuf Manji kama Mwenyekiti wao.
Karia amesema kwamba Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anatakiwa awe Mwenyekiti wa klabu ya Ligi Kuu, Sanga amepoteza sifa za kuwa kiongozi Mkuu wa bodi hiyo.
"Tulipokea barua Julai 12 kutoka klabu ya Yanga ikidai kuwa Sanga hatambuliki kama Mwenyekiti wa klabu hiyo, wao Yanga wanamtambua Yussuf Manji ndiye Mwenyekiti wa klabu hiyo na katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi unatakiwa Uwe Mwenyekiti wa klabu yako," amesema Karia 
Katika hatua nyingine, Karia amesema Kamati ya Utendaji imempitisha ras... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More