COASTAL UNION YANG’ARA MLANDIZI, YAIPIGA RUVU 1-0, BIASHARA UNITED HAITISHI NYUMBANI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

COASTAL UNION YANG’ARA MLANDIZI, YAIPIGA RUVU 1-0, BIASHARA UNITED HAITISHI NYUMBANI

Na Sada Salmin, MLANDIZI
TIMU ya Coastal Union imepata ushindi wa 1-0 ugenini kwa Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika jioni ya leo.
Ushindi huo umetokana na bao la kujifunga la beki wa zamani wa Coastal Union Tumba Swedi dakika ya 64 akiwa katika harakati za kuokoa.
Na kwa matokeo hayo Coastal Union inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Juma Mgunda inafikisha pointi tisa baada ya kucheza mechi sita, wakati Ruvu inabaki na pointi zake mbili baada ya kucheza mechi tano.   
Mechi nyingine ya leo, Biashara United imelazimishwa sare ya bila kufungana na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Karume Musoma mkoani Mara.

Hiyo inakuwa sare ya tatu mfululizo katika mechi za nyumbani baada ya kutoka 0-0 pia na Azam FC na 1-1 na Kagera Sugar katika mechi zake mbili zilizopita Uwanja wa Karume.
Kwa matokeo hayo, BUM inafikisha pointi sita katika mechi ya sita, wakati JKT Tanzania ambayo nayo kama Biasha... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More