COASTAL UNION YAWEKWA CHINI YA UANGALIZI KWA VURUGU ZA MASHABIKI, WAKIRUDIA MKWAKWANI UNAFUNGIWA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

COASTAL UNION YAWEKWA CHINI YA UANGALIZI KWA VURUGU ZA MASHABIKI, WAKIRUDIA MKWAKWANI UNAFUNGIWA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeamua timu ya Coastal Union ya itakuwa kwenye uangalizi kwa mechi mbili zijazo za Uwanja wa nuyumbani, Mkwakwani mjini Tanga kufuatia tuhuma za mashabiki wake kuvamia uwanjani. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Boniface Wambura Mgoyo amesema hayo yamefikiwa katika kikao cha Bodi Oktoba 5, mwaka huu kupitia taarifa na matukio katika mechi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinazoendelea hivi sasa na taarifa mbalimbali. 
Mashabiki wa wanadaiwa kuingia uwanjani baada ya mechi namba 24 dhidi ya KMC FC iliyomalizika kwa sare ya 0-0 Septemba 1, 2018 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, huku waamuzi na wachezaji wakiwa bado hawajatoka, kitendo ambacho ni hatari kiusalama.
“Kamati imeamua kuwa Coastal Union itakuwa kwenye kipindi cha uangalizi kwa mechi mbili zijazo, na iwapo washabiki wataendelea kuingia ndani ya uzio, timu hiyo itafungiwa kuutumia uwanja huo,... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More