Conor McGregor apokea kipigo cha karne kutoka kwa Khabib ‘alitukana dini yangu, nilikuwa tayari kufa’ (+video) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Conor McGregor apokea kipigo cha karne kutoka kwa Khabib ‘alitukana dini yangu, nilikuwa tayari kufa’ (+video)

Baada ya kukaa kimya kwa miaka miwili mfululizo kwenye mapambano ya UFC, Mwanamasumbwi Conor McGregor leo alfajiri amepokea kipigo cha mbwa koko kutoka kwa Mrusi Khabib Nurmagomedov.Khabib  alikuwa anatetea mkanda wake wa Lightweight katika pambano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa T-Mobile Arena jijini Las Vegas nchini Marekani.


Mrusi huyo anaendeleza rekodi yake ya ushindi na mpaka sasa amepigana mapambano 27 bila kupoteza hata moja. Pambano la leo ni pambano lake la kwanza kutetea mkanda wake baada ya kuuchukua toka kwa McGregor aliyevuliwa ubingwa baada ya kukaa nje kwa kipindi kirefu akijiandaa na pambano la ndondi dhidi ya Floyd Mayweather.


Hata hivyo, Khabib hakupewa mkanda huo jukwaani, hii ni baada ya vurugu kubwa kuibuka kwenye ukumbi huo jambo ambalo liliwalazimu walinzi na polisi kuingilia kati baada ya Khabib kuruka nje ya uwanja na kuivamia timu ya McGregor.


Khabib kwenye mkutano wake na waandishi wa habari baada ya pambano, aliomba radhi na amesema ushindi wake uli... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More