COUTINHO ABADILISHIWA JEZI BARCELONA, APEWA NAMBA YA FIGO - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

COUTINHO ABADILISHIWA JEZI BARCELONA, APEWA NAMBA YA FIGO

KIUNGO Philippe Coutinho amepewa jezi namba saba (7) Barcelona kutoka namba 14 aliyokuwa anavaa tangu amejiunga na timu hiyo Januari mwaka huu akitokea Liverpool.
Jezi hiyo ambayo imewahi kuvaliwa na magwiji kama Luis Figo, David Villa na Henrik Larsson, awali ilikuwa inavaliwa na Arda Turan, ambaye ametolewa kwa mkopo Istanbul Basaksehir na kuiacha wazi.
Mara ya mwisho Coutinho kuvaa jezi namba 7 ilikuwa katika msimu wake wa mwisho Inter Milan kabla ya kujiunga na Liverpool mwaka 2013. Alipokuwa Liverpool, alikuwa anavaa namba 10. 

Philippe Coutinho amepewa jezi namba saba (7) Barcelona kutoka namba 14 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na Barcelona Januari kwa dau la Pauni Milioni 145, na mara moja kugeuka kuwa mchezaji muhimu Nou Camp, akifunga mabao 10 katika mechi 22 katika nusu ya pili ya msimu uliopita.
Pia aling'ara katika Kombe la Dunia akifunga mabao mawili kabla ya Brazil kutolewa katika Robo Fainali na Ubeligiji.
Mchezaji aliyedumu kwa mu... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More