Cristiano Ronaldo asababisha wafanyakazi wa Fiat kuitisha mgomo - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Cristiano Ronaldo asababisha wafanyakazi wa Fiat kuitisha mgomo

Cristiano Ronaldo ametua Juventus na sasa kinachosubiriwa ni nyota huyo wa timu ya taifa ya Ureno kusaini kandarasi tu tayari kwa kuanza kuitumikia Juventus.


Moja ya masuala ambayo ni gumzo sana kwa sasa ni uwezo wa kipesa ambao Juve wameouonesha kwa Ronaldo kwani sasa nyota huyo ataigharimu zaidi ya shilingi bilioni 84 klabu ya Juventus kwa mwaka achana na £105m waliyomnunulia.


Sasa baada ya dili hilo kutangazwa, wafanyakazi wa kampuni ya magari ya Fiat ambao ni moja ya wamiliki wa klabu ya Juventus wameitisha mgomo wakipinga kiasi ambacho Fiat watahusika katika kumlipa Cr7.


Imetangazwa kwamba wafanyakazi hao watakuwa na mgomo ambao utaanza tarehe 15 kupinga kile walichoeleza kama kupambana kwa kutumia nguvu kubwa lakini mwisho wa siku kampuni inatumia pesa kumlipa mchezaji mmoja.


Wafanyakazi hao wameeleza kwamba maisha yao sio marahisi na wamewekeza nguvu zao zote kwenye kazi na walifikiri kampuni ingefikiria kuhusu mishahara mipya na tofauti na matarajio yao kampuni imewekeza kwa C... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More